.

Translate to your own native language.

Friday, 22 May 2020

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza kuwa vyuo vikuu vyote nchini humo vitafunguliwa kuanzia Juni 1, 2020 na mtihani wa taifa pamoja na ualimu kufanyika kuanzia June 29, 2020 hadi July 16, 2020.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Wanafunzi wa kidato cha sita nchini Tanzania ambao wanakaribia kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya sekondari nchini humo pia watarejea shuleni siku hiyo.

Magufuli amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kwa kuwa kasi ya ugonjwa wa corona imepungua nchini Tanzania.

"Hali ya ugonjwa wa Corona nchini imeshuka sana hivyo, sisi kama serikali tumeamua kufungua vyuo vyote Juni 1, 2020 kwahiyo Wizara zinazohusika zijiandae ili vyuo vitakapofunguliwa isitokee kero zingine," ameeleza Magufuli.

Magufuli hata hivyo amesema wanafunzi wengine bado kunahitajika muda wa kufanya tathmini.

"Kwa shule za msingi na madarasa mengine ya sekondari tujipe muda kidogo...tutatathmini maendeleo ya wengine waliofungua kwanza. Hawa wa chuo kikuu ni watu wazima, wanajitambua," amesisitiza rais Magufuli.

Taasisi zote za elimu nchini Tanzania zilifungwa katikati ya mwezi Machi mara baada ya Tanzania kuthibitisha mgonjwa wa kwanza wa virusi vya corona nchini humo.

Ligi Kuu kurejea Juni 1 pia

Rais Magufuli pia ameatanzaza kuwa tarehe hiyo ya Juni 1 pia ndiyo michezo yote ikiwemo Ligi Kuu ya Kandanda itarejea nchini humo.

Michezo ni muhimu hivyo tumeamua pia kufungua michezo kuanzia Juni 1, 2020, taratibu za kuangalia na kushangilia mpira zitapangwa vizuri na Wizara ya Afya pamoja na Wizara ya Michezo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dkt Hassan Abbas amesema kupitia mtandao wa Twitter kuwa baada ya kauli hiyo ya rais sasa ni rasmi kwa timu zote kuanza mazoezi.

Mapema wiki hii Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini Tanzania (TFF) Wallace Karia aliiambia BBC kuwa wanaendelea na maandalizi ya ndani wakisubiri mwongozo rasmi wa serikali.

Karia alisisitiza kuwa michezo ya ligi itakaporejea, mashabiki hawataruhusiwa uwanjani.

Kasi ya Corona Tanzania

Rais Magufuli pia amesema kati ja Mei 27 na 28 ndege za watalii zitaanza kuingia Tanzania.

Hayo ameyasema asubuhi ya leo katika Ikulu ya Chamwino Dodoma kwenye hafla ya kuwaapisha viongozi kadhaa aliowateua hivi karibuni akiwemo Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel pamoja na mabalozi kadhaa.

Rais Magufuli alitangaza Jumapili iliyopita na kusisitiza hii leo kuwa kasi ya corona imepungua Tanzania.

"Kwa taarifa za leo wagonjwa wamepungua, Amana ilikuwa ina watu 198 leo wamebaki 12 tu, Mlogonzila ilikuwa inalaza watu 30 leo wamebaki 6, Hospitali ya Kibaha kulikuwa na Wagonjwa 50 leo wamebaki Watu 22," rais Magufuli alisema siku ya Jumapili.

Mpaka sasa, watu 509 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona nchini Tanzania, huku 183 wakipona na watu 21 kufariki dunia.

Mara ya mwisho kwa Tanzania Bara kutangaza takwimu mpya za corona ilikuwa wiki mbili zilizopita Aprili 29, huku Zanizbar ikitoa takwimu mpya kwa mara ya mwisho wiki moja iliyopita Mei 7.

Kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika (Africa CDC) kilichopo chini ya Umoja wa Afrika (AU) wiki ilopita kiliitaka Tanzania kutoa takwimu mpya za mwenendo wa ugonjwa wa corona nchini humo.

Mkurugenzi wa Africa CDC, Dkt John NkengasongHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMkurugenzi wa Africa CDC, Dkt John Nkengasong

Mkurugenzi wa Africa CDC, Dkt John Nkengasong Alhamisi Aprili 14 alisema kuwa kituo chake kwa kutumia takwimu hizo kipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa kuipatia msaada wa kitaalamu na kiufundi unaohitajika.

"Hili ni janga kubwa kwa bara (Afrika) lote na dunia kwa ujumla… hivyo ni kwa faida ya Tanzania kutoa takwimu kwa wakati ili tufahamu mapungufu yapo wapi na tuwasiadie kadri itakavyohitajika," amesema Dkt Nkengasong katika mkutano na wanahabari kwa njia ya mtandao.










Popular Posts this week.

Blog Archive