Wednesday, 24 June 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI TRA 4 Julai, 2020

Tanzania Revenue Authority

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/224

Katibu wa Sekretarietiya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba yaMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili wa mchujo unatarajiwa kufanyika tarehe 4 Julai, 2020 nakufuatiwa na usaili wa mahojiano ambao tarehe itapangwa baadae.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i.Usaili wa mchujo utafanyika tarehe 04Julai, 2020kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;

ii.Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask) na kuzingatia masharti mengine ya kujikinga na COVID 19 KAMA YALIVYOAINISHWA NA WIZARA YA AFYA awapo eneo la usaili,

iii.Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

iv.Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja naamaKitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazicha taasisi inayojulikana, Kitambulishocha Uraia ,Hati ya kusafiria au Leseni ya Udereva
v.Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;vi.Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) 

HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
vii.Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
viii.Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
ix.Kwa waombajiwaliosomanje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA,NACTE auTCU);
x.Waombaji kazi ambao majina yao hayaonekanikatika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
xi.Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

KUSOMA MAJINA PAKUA PDF HAPA Download